Pilau ni mchanganyiko wa mchele na viungo mbalimbali,chakula hiki ni
kitamu sana na watu hupendelea sana kupika wakati wa sherehe. Unaweza
ukala pilau na kitoweo chochote kile unachopenda mfano mimi nimependa
kula na njegere,kachumbali na matunda.
Mahitaji
- Mchele
- Kuku
- Mafuta
- Vitunguu maji
- Carrots
- Pilipili hoho
- Tangawizi
- Viungo vya pilau
- Vitunguu saumu
- Chumvi
- Nyanya 3
Maelekezo
- Mkate kuku umpike na chumvi akiiva hakikisha supu ya kupikia chakula inatosha.
- Menya vitunguu maji ukatekate,vitunguu saumu menya utwange na
tangawizi,menya carrots uzikwangue na pilipili hoho ukatekate mwisho
nyanya pia menya ukate kate.
- Bandika sufuria utie mafuta, ikichemka tia vitunguu uvikaange.
Vikianza kubadilika rangi weka vitunguu saumu na tangawizi mbichi koroga
kidoga weka pilipili hoho na carrots.
- Kaanga kidogo kisha weka nyanya acha ziive na vipande vya kuku koroga kama dk tano weka viungo vya pilau.
- Weka mchele koroga kisha tia chumvi na umimine supu ile ya kuku kwenye wali.
- Koroga kisha funika acha chakula chako kiive baada ya dk kumi
angalia chakula chako kama maji yamekauka kigeuze palia baada ya dakika
kadhaa angalia tena hapo chakula chako kitakua tayari kuliwa.
- Pilau yako itakuwa tayari kwa kuliwa
- Mpendwa wangu karibu mezani
Post a Comment