- 500 gram za wali ulioiva.
- 2 kijiko kikubwa cha chakula kitunguu swaumu kilichosagwa.
- 4 au 5 mbegu nzima za kitunguu swaumu kilichomenywa (sio lazima).
- 4 miti ya majini ya kitunguu maji chop chop.
- 5 gram chumvi.
- 1 kijiko kikubwa cha chakula cha siagi (butter).
Jinsi ya kupika
- Weka siagi kwenye kikaango kilichokwisha pata moto ili iyeyuke kisha weka mbegu za kitunguu swaumu ziendelee kuiva.
- Kaanga mpaka iwe ya kahawia hakikisha haiunguwi kisha toa hizo mbegu na weka pembeni..
- Katika kikaango hicho hicho, weka kitunguu swaumu cha kusagwa na majani ya kitunguu maji mabichi yaliyo katwa katwa
- Mchanganyiko wako ukishalainika na kutoa arufu nzuri, chukua wali wako na weka katika kikaango na hakikisha una changanya haraka haraka
- Weka zile mbegu za kitunguu swaumu ulizokaanga mwanzo na uendelee kuchanganya ili iweze changanyika vizuri.
- Chakula hiki unaweza kula na mchuzi au mboga za aina yeyote.
- Pia chakula hiki kinaweza kuliwa pamoja na tunda la parachichi ili kuongeza ladha ya chakula chako
Post a Comment