Jinsi ya Kuandaa Pilau


Pilau ni chakula maalumu kwa waswahili wa pwani ya afrika mashariki ambapo mchele huchanganywa na viungo Mbalimbali na hupikwa  kwa mchanganyiko wa nyama, Kuku au Samaki, na pia ni chakula chenye heshima kubwa na ambacho haupaswi kukukosa wakati wa sherehe mbalimbali kubwa.

Mahitaji

  •        Mchele nusu kilo , Uliosafishwa  kwa maji
           Viazi nusu kilo – menya, na uvisafishe kwa maji
           Nyama Nusu kilo, Kuku au nyama ya samaki.
           Kikombe kimoja cha mafuta ya alizeti (au mafuta yeyote ya kula)
           Vikome 4 vya maji ya moto au Supu
           Kitunguu 1, kilicho menywa
           Vijiko 5 vya karafuu iliyosagwa
           Tangawizi  iliyosagwa (kijiko 1 au 2)
           Nyanya 2, zilizokatwa katika vipande vidogovidogo
           Viungo vya Pilau Vijiko 2 (Vilivyosagwa)
           Chumvi na Pilipili kwa ajili ya Kuongeza ladha nzuri

  • Maelekezo
    Chemsha nyama pamoja na tangawizi kwa dakika 10. Weka Viazi na uache vichemke kwa dakika tano  na epua uweke pembeni (tenganusha supu hivyo unaweza kutumia baadaye)
    Pasha mafuta  na weka vitunguu hadi vibadilike rangi na kuwa brown, weka vitunguu na Viungo vya pilau na changanya kwa dakika 1, kwa moto mdogo.
    Weka nyanya, nyama pamoja na viazi na Koroga
    Weka mchele na hakikisha mchanganyiko wa kila kitu umechanganyika vizuri kabla ya kuweka supu au maji ya moto, na koroga vizuri.  
    Weka chumvi na pilipili kwa ajili ya Kuongeza ladha, alafu funikia chakula chako kiive kwa moto wa kawaida

    Chakula chako kikianza kukaukia, Punguzia moto kwa chini, na Funikia Pilau yako, na iache iive kwa dakika 10

    Hapo pilau yako itakuwa tayari!

    Pendezesha Pilau yako kwa kachumbari na Pilipili ya maembe

    Na ndizi pia inaweza ikatumika ili Kuongeza ladha zaidi

  • Baadhi hupendelea kula Pilau kwa tomato na nyama ya kuku kwa pembeni ambayo nayo ni vizuri zaidi


Post a Comment

[blogger]

MKRdezign

Blogger Widgets

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget