Mahitaji
- Kuku 1
- Mafuta ya kula
- Kikombe 1 cha kahawa
- Kitunguu saumu cha unga vijiko 3 vya chakula
- Malimao 4
- Paprika nusu kijiko cha chai
- Unga wa kitunguu saumu kijiko 1 cha chai
- Vitunguu maji 2 vikubwa
- Chumvi kijiko 1 na nusu cha chai
- Pilipili manga kijiko 1 cha chakula
- Maji kikombe kidogo kidogo
- Kijiko 1 kidogo cha Unga wa haradali (Mustard powder)
- ½ kijiko cha chai cha thyme
- ½ kijiko cha chai cha lemon zest
Maelekezo
Huyu kuku ni mtamu, na ni chakula bora sana kwa familia. Kama unahitaji kujiramba na kuvinjari, basi hapa ndio umefika.
- Changanya viungo (kasoro mafuta ya kula na ndimu) kwenye blender. Saga ili upate mchanganyiko sawia. HIfadhi pembeni.
- Andaa kuku – unaweza kumkata vipande au ukamuacha mzima kisha msafishe na mkaushe kwa kitambaa safi.
Kama unataka kuoka kuku, hakikisha kuwa huondoi ngozi. Ngozi husaidia kumfanya kuku aive vizuri
- Kwenye mfuko wa nylon au plastic weka mchanganyiko wa viungo vyote kisha weka kuku na umchanganye vizuri ili apate kuingia viungo.
- Hifadhi mfuko wenye kuku kwenye fridge kwa takribani masaa 6 hadi 7
- Ukiwa tayari kuandaa kuku, toa kwenye mfuko, panga kwenye bakuli (sinia au chombo chochote) la kuokea kwenye oven.
- Washa oven na uipashe moto kwenye nyuzi 300°F (150°C)
- Kamua limao kwenye chombo kikavu. Changanya maji ya limao na mafuta ya kula kwa pamoja upate mchanganyiko sawia. Kata vizuri vipande vya limao lililobaki na weka pembeni, usitupe.
- Mwaga mchanganyiko juu ya vipande vya kuku vizuri. Mloanishe ili apate kuwa na unyevunyevu mzuri.
- Panga vipande vya limao kwenye bakuli vizuri pembeni ya vipande vya kuku.
- Tega oven kwa dakika 45 na weka kuku ili apate kuiva. Unaweza kuangalia kama anaungua ili kumgeuza.
- Baada ya dakika 45, toa kuku. Angalia kama ameiva vizuri ndani.
- Unaweza kula chakula hiki na ugali, wali, ndizi au vinginevyo. Unaweza pia kula kama kitafunwa kizuri na kinywaji baridi.
- Hapo tayari kuku wetu kwa kuliwa karibu mezani na jilambe
Post a Comment