MAHITAJI:
1.Unga wa Ngano 200gm
2.Hiliki punje 5
3.Yai 1
4.Maziwa kikombe kidogo cha chai 1 na robo
5.Sukari kijiko cha chakula kimoja 1
6.Mafuta Nusu Kikombe
MAANDALIZI:
1.Chukua bakuli kubwa kiasi chekecha unga weka pembeni
2.Menya hiliki na uzitwange vizuri
3.Vunja yai kwenye kibakuli lipige na umma kama unataka kulikaanga weka pembeni
4.Chukua maziwa weka kidogo kidogo kwenye unga huku ukiuchanganya na mchapo au upawa mpaka uwe na uzito kiasi hakikisha hauwi mwepesi sana wala mzito sana
5.Weka hiliki ,sukari na yai kisha changanya vizuri mpaka uji wako uchanganyike na vitu vyote
1.Weka chuma(frying pan) chako jikoni na mafuta kijiko kimoja yaeneze kwenye chuma chote
2.Tumia upawa chota miko miwili au zaidi inategemea na ukubwa wa chuma chako na ieneze kwenye chuma chote
3.Ueneze mkate wako kwenye chuma upate duara na unakuwa mwembamba kiasi
3.Acha kwa dakika 4 mpaka uone mkate wote umekauka ule umaji maji wa ubichi haupo
4.Ugeuze upande wa pili uache kwa dakika 3 au 4 ukauke
5.Chota mafuta kijiko kimoja weka chini ya mkate wako huku ukiuzungusha mpaka upate rangi ya kuvutia
6.Ugeuze kisha utoe weka kwenye sahani
7.Rudia njia hizi mpaka umalize uji wote
8.Weka mezani kula na chai ya maziwa, ya rangi, juice au kinywaji chochote
ANGALIZO ZAIDI:
1.Yai ni muhimu usipoweka mikate inaganda kwenye chuma
2.Kama hutaki rangi ya kahawia usiiache kwa muda mrefu baada ya kuweka mafuta
3.Tumia Nonstick Frying Pan kwa kuhofia kugandisha mikate mara kwa mara
4.Ili upate mikate mizuri ya kuvutia hakikisha moto ni wa wastani ukipikia moto mkubwa zinakua mbaya
Post a Comment