Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu amesema ana
kila sababu ya kuzungumza japo kwa kifupi jitihada mbalimbali
zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na serikali katika
kuimarisha usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini.
Makamu
wa Rais amesema kuwa serikali ina sera kuendeleza wanawake,huku akisema
kuwa sheria ya ardhi za mwaka 1999 ambazo husimamia haki za wanawake
katika kumiliki ardhi.
"Leo
katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Mimi kama mwanamke na
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nina kila sababu ya
kuzungumza japo kwa kifupi jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na
zinazoendelea kuchukuliwa na serikali katika kuimarisha usawa wa
Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini.
"Serikali
inayo Sera ya kuendeleza Wanawake, Sheria za ardhi za mwaka 1999 ambazo
husimamia haki za wanawake katika kumiliki ardhi.
"Sera ya elimu bure inayotekelezwa na serikali ya Awamu ya Tano imetoa fursa kwa watoto wengi wa kike kuandikishwa shuleni.
"Kuboreshwa
kwa huduma za kijamii kama vile kujengwa zahanati na vituo vya afya na
usambazaji wa maji vimempunguzia mwanamke usumbufu na hivyo kumpa muda
wa kutosha kufanya shughuli za maendeleo.
"Usambazaji
umeme vijijini kwa kiasi kikubwa umesaidia wanawake wengi
kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato.
"Uwezeshaji
wa Wanawake kwa kuwapatia asilimia 5 ya mapato ya halmashauri na
asilimia 30 ya zabuni za halmashauri kumewawezesha wanawake wengi
kufanya biashara na hatimaye kuwa na uhakika wa kipato .
"Serikali
kuendelea kuhimiza taasisi za kifedha kutoa mikopo yenye riba nafuu ili
kuwawezesha wanawake wengi kunufaika na mikopo hiyo.
"Kurasimisha
vikoba pamoja na kuwashawishi wanawake wengi zaidi kujiunga na mifuko
ya hifadhi ya jamii ili kuweza kunufaika na mafao na mikopo itolewayo na
taasisi hizo.
"Kauli Mbiu:Kuelekea Uchumi wa Viwanda tuimarishe usawa wa kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini."
Post a Comment