“Weupe wa penzi lako ni kama mwezi angani.Ucheshi na mahaba yako
nifananishe na nini? Kupata mfano wako hatotokea amini. Elewa mimi ni wako sikuachi asilani”
“Najiuliza kila leo hivi ni mimi tu kimeo katika dunia hii ya leo maana
kila leo nayempata huishia kunipa ahadi kila leo, mpenzi kila siku waniaidi
mara nitakupa leo mara kabla ya machweo, hivi ni lini utanipa jibu la uhakika
nakunipa mapenzi ya uhakika nipate farijika? Nakupenda mpenzi”
“Hakika mtoto umeumbika mithili ya malaika japo mbinguni sijafika lakini
nauhakika kwa kila mwanaume aliyeumbika na kukamilika akikuona lazima udenda
utamtoka, naomba japo yako dakika nipate kukueleza moyoni yaliyonifika kwani
siwezi tena kuficha jinsi navyokupenda, nakupenda amini kwako nimefika!”
“Nimezunguka pande zote za Tanzania macho nikiangaza kumsaka mrembo
wakumkabidhi yangu nafsi na kulila tunda lake kwa nafasi huku nikimpa mahaba
yangu ya dhati na sikuwahi kuhisi kama wewe ndiye ungeiteka yangu nafsi,
nakupenda sweetie.”
“Mpenzi nimekumiss jamani, sipati meseji wala simu sijui kwanini,
nikikumbuka tunayofanyaga kitandani, natamani ungekuwa nami pembeni nakunipa
mahaba yasiyo kifani, nakupenda si utani hani”
“Sijui nikuekleza namna gani uelewe yaliyionijaa moyoni kwani kila
nifikiriapo kwanini una walakini na hutaki kuniamini kama wewe pekee ndiye
ninayekupa mahaba yangu makini, mpenzi rudisha yako imani ni wewe pekee
nayekupenda hapa duniani!”
“Ukweli lazima nikwambiye kwa kuwa sina kimbilio nakupenda kijana
mwenzio sijui kwanini hutaki kukisikia changu kilio, namwomba Mungu kila
kukicha usikiye changu kilio, nakupenda na kama kukueleza hili nakukosea
nisamehe kwani si langu kusudio,luv u mwaah.”
“Naamini uatakuwa umerejea kwenye yako makazi na umechoka na kazi,
tafadhali badili yako mavazi , bafuni ingia upate maji kujimwagia, natamani
kuja kukusaidia mgongo kuusugua na chakula kukuandalia lakini siku haijawadia,
nakupenda dear!”
“Kwa kawaida busu la mafanikio hubusiwa usoni, busu la amani hubusiwa
mashavuni, busu la upendo hubusiwa mdomoni, busu la mapenzi hubusiwa shingoni,
Je wapi nikubusu ili ulale kwa raha sweet ?”
“Mapenz si pombe lkn yanalewesha,wala c dawa lkn yanaponyesha,wala c
maradhi lkn yanaua,wala c kifo lkn yanaliza,wala si katuni lkn
yanafurahisha,wala c fimbo lkn yanaumiza.Ni mimi tu mwenye mapenzi ya kweli
kwako,Nipende daima mpenzi!!”
“USikimbie nyuki ukakosa asali, utamu wa samaki ni kula na
wali,usizidishe siki akawa mkali. Ni mimi niliye na dhiki nakujulia tu
hali.Je,unaendeleaje sakafu wa moyo wangu?”
“Hakika nakwambia mpenzi wanaokutamani ni wengi lakini ni mimi tu mwenye
hayo mapenzi ya kweli.ziba masikio na usiwasikilize,nia yao
watugombanishe.Nipende daima laaziz wangu!!”
Post a Comment