ROAST YA MAINI

Mahitaji

  • Maini ½ kilo
  • Nyanya 4
  • Kitunguu 1
  • Karoti 1
  • Pilipili hoho 1
  • Ndimu 1
  • Chumvi
  • Mafuta ya kula

Maelekezo

  • Anza kutayarisha maini kwa ufasaha. Ondoa tabaka (ngozi ya juu) ya maini ambayo huwa hailiwi. Osha na kata vipande kwenye ukubwa unaopenda.
  • Nyunyuzia ndimu kwenye vipande vya maini na kisha weka chumvi. Changanya vizuri ili vipande kuchanganyika sawia.
  • Andaa viungo kwa kuosha na kuvikata vipande vidogo – nyanya, pilipili hoho, karoti na vitunguu.
  • Weka mafuta kwenye sufuria, chungu au kikaangio unachotumia kupikia maini.
  • Weka maini. Yakaange hadi yaive.
  • Weka kitunguu, koroga ili viive vizuri.
  • Weka pilipili hoho n a karoti. Koroga kwa dakika 2 hadi 3.
  • Weka nyanya. Koroga kiasi.
  • Kama chumvi haitoshi, ongeza chumvi. Koroga na kisha funika na mfuniko ili nyanya ziiive.
  • Baada ya dakika 5 – 8 unaweza kutoa mboga kwa kuwa imeiva.
  •  Pia Mboga hii waweza kutumia kwa wali au ugali 

Post a Comment

[blogger]

MKRdezign

Blogger Widgets

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget