WALI WA VIUNGO
Mahitaji
- Mchele nusu kg
- Vitunguu maji 3
- Karoti 4 kubwa
- Mafuta
- Chumvi kiasi upendavyo wewe
- Pilipili hoho 1
- Kitunguu saumu 1
- Pilipili manga nusu kijiko cha chai
- Iliki iliyosagwa nusu kijiko cha chai
Maelekezo
- Osha mchele,uache kwenye maji. Menya karoti katakata, vitunguu maji menya ukate kate.
- Kitunguu saumu menya kiponde na pilipili hoho katakata.
- Bandika sufuria jikoni, weka mafuta na vitunguu maji koroga kama dakika 2 weka vitunguu saumu, usiache kukoroga.
- Weka karoto na pilipili hoho, weka iriki na pilipilimanga kisha funika.
- Weka mchele na chumvi, weka na maji kama kikombe kimoja na nusu cha chai.
- Funika maji yakikauka, usiugeuze ibanike baada ya dakika 10
uangalie, ugeuze onja kama bado una kiini ongeza maji kama vijiko 5 vya
chakula.
- Funika ukija kuangalia utakua umeiva.
- Sasa jilambe.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget
Post a Comment