Chakula rahisi kuandaa cha viazi na meatballs. Kinapikwa kwa nazi na maziwa. Kinaweza kuliwa na mkate au wali,.
Mahitaji
- Meatballs 8
- Nazi ½
- Maziwa ya mgando 1/8 lita
- Karoti 1
- Kitunguu maji 1
- ½ kijiko cha chai cha chumvi
- Kijiko 1 cha kitunguu saumu
- Pilipili hoho ya kijani ½
- Pilipili hoho nyekundu ½
- Nyanya 4
Maelekezo
- Menya viazi, osha na kisha kata vipande vidogo vidogo. Bandika
jikoni na maji ya kutosha. Ongeza chumvi na funika vipate kuchemka,
takribani dakika 10 hadi 15.
- Injika chungu kwenye jiko tofauti, weka mafuta ya kula mengi na acha yapate moto.
- Andaa viungo yako – kitunguu, pilipili hoho, nyanya, karoti na kitunguu saumu.
- Mafuta yakipata moto, weka meatballs zako na zigeuze kila baada ya
muda hadi ziive vizuri pande zote. Hakikisha zimeiva vizuri ndani. Kisha
zitoe na weka kwenye chombo pembeni zipate kupoa.
- Viazi vikiiva, ipua na injika sufuria jikoni. Weka mafuta na subiria yapate moto vizuri.
- Weka kitunguu maji, koroga kiasi. Ongeza kitunguu saumu huku
unaendelea kukoroga hadi vibadilike rangi na kuwa ya udongo iliyopauka.
- Ongeza nyanya, koroga. Funika kidogo ipate kuiva na kulainika. Baada
ya dakika 5 au 7 ponda nyanya na kisha ongeza viungo vilivyobaki kwa
zamu – pilipili hoho, karoti, kisha tui la nazi na mwisho kabisa maziwa
kidogo. Koroga na kisha funika vichemke vizuri. Bakisha tui kidogo.
- Sauce yako ikishaiva, ongeza viazi kwenye mchanganyiko, koroga na acha viendelee kuiva. Ongeza tui lililibaki na kisha koroga.
- Mchanganyiko ukishaiva, weka meatballs, koroga kiasi, acha ichemke
kwa dakika 4 hadi 6 kisha ipua; Usiache muda mrefu sababu nyama
italainika sana na kubomoka.
- Chakula chako kitakuwa tayari kwa kuliwa
Post a Comment