February 2018



JESHI la Polisi mkoani Mwanza, linamshikilia Soli Mkanzabe (24), mkazi wa mtaa wa Nyegezi kwa tuhuma za kumnajisi mtoto wa miaka minne (jina limehifadhiwa) na kumsababishia majeraha na maumivu makali katika sehemu za siri.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna (DCP) Ahmed Msangi, katika taarifa aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari, alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo juzi majira ya saa 10 jioni katika maeneo ya mtaa wa Password kata ya Nyegezi, Nyamagana mkoani hapa.

“Inasemekana mtuhumiwa alikuwa akiishi jirani na nyumbani kwao mtoto. Inadaiwa kuwa majira tajwa hapo juu, mtuhumiwa alifika nyumbani kwao mtoto na kumkuta akicheza na wenzake kisha alimwita waende wote chumbani kwake.

Mtoto alimfuata mtuhumiwa na kwenda naye chumbani na baadaye mtuhumiwa alifanyia mtoto ukatili wa kumbaka na kumsababishia maumivu makali katika sehemu za siri huku mtuhumiwa akimwonya mtoto kuwa asiseme kwa mtu yeyote juu ya jambo hilo,” alisema DCP Msangi katika taarifa hiyo.

Msangi alisema baada ya mtoto kufanyiwa ukatili huo, alikaa kimya bila kumwambia mtu yeyote hadi mama yake aliporejea kutoka kazini.

Kamanda Msangi alisema wakati mama yake akienda kumwogesha, ndipo alipogundua kuwa mtoto amefanyiwa unyama huo kisha alitoa taarifa kituo cha polisi.

Alisema baada ya kutoa taarifa, polisi walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa.

Kutokana na kumkamata huko, DCP Msangi alisema polisi wako katika upelelezi na mahojiano namtuhumiwa na kwamba uchunguzi ukikamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Kuhusu mtoto huyo, Msangi alisema alipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana na kwamba hali yake inaendelea vizuri.



Hatimaye Bosi wa Wasafi Classic Baby (WCB) Diamond Platinumz amepata leseni ya kuziweka hewani redio na televisheni za Wasafi zilizobatizwa jina la ‘Wasafi Radio na Wasafi TV’.

Diamond amevuka maji na kuzipata leseni zake visiwani Zanzibar ambapo alikabidhiwa na Wizara ya Habari, Tamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar, Rashid Ali Juma.

Mkali huyo wa ‘Sikomi’ jana aliwashirikisha mashabiki wake habari hiyo njema iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu, siku chache baada ya kuonesha picha akiwa anajaribu mitambo ya mradi huo mpya.

Kupitia Instagram, ameandika ujumbe akiambatanisha na picha za leseni hizo, akiishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.




WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuwalinda watoto wa kike na ndiyo maana tunawataka watoe taarifa za watu wanaotaka kuwakwamisha kimasomo kwa watendaji wa vijiji kwenye maeneo yao.

Alitoa agizo hilo jana (Jumatatu, Februari 26, 2018) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wakazi wa wilaya ya Masasi akiwa katika siku ya kwanza ya  ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara.

Waziri Mkuu alisema watoto wa kike wanatakiwa kuheshimiwa katika jamii kwa kuachwa waendelee na masomo yao bila ya usumbufu wa aina yoyote na atakayebainika kukatisha masomo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Alisema Serikali  itatoa adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtu atakayekatisha elimu ya mtoto wa kike iwe kwa kumuoa, kumpa ujauzo na hata ukikutwa naye nyumbani kwako, katika nyumba ya wageni.

“Tukikukuta na binti wa shule katika kona isiyoeleweka tunakukamata na kukuchukulia hatua za kisheria. Ole wenu vijana, mkibainika mmewapa mimba mabinti wanaosoma, adhabu yake ni miaka 30 jela.”

Waziri Mkuu alisema kwa wazazi au walezi watakaowaozesha watoto kike ambao bado wanafunzi na kwa upande wa wazazi watakaomsindikiza mtoto kwenda kuoa mwanafunzi wote watachukuliwa hatua za kisheria.

Pia Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi wote kusoma kwa bidii ili watimize ndoto zao na wasikubali kushawishika kwa sababu watashindwa kufikia masomo yao.


Mamlaka nchini Nigeria imesema imeongeza nguvu ya ndege za kivita ili kuweza kuwasaka wanafunzi wasichana waliotekwa Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Serikali inasema takriban wasichana 110 hawajulikani walipo baada ya wanamgambo wa kiislam kuwateka katika shule yao iliyopo Dapchi.
Mapema serikali ya kijiji hicho ilililaumu jeshi kwa kushindwa kuchukua hatua hata baada ya kupewa taarifa.
Rais Muhammadu Buhari ameelezea tukio hilo kama janga la taifa.
Hasira zimekuwa zikiwapanda wazazi wa wasichana hao huku kukiwa na ripoti kuwa wanajeshi walikuwa wameondolewa kutoka kwa vizuizi vikuu vya Dapchi mwezi uliopita.
Dampchi ambao ni mji ulio kilomita 275 kaskazini magharibi wa Chibok, ulishambuliwa siku ya Jumatatu, na kusababisha wanafunzi na walimu kutoka shule moja ya serikali kukimbiliaa vichakani.
Wenyeji wanasema vikosi vya jeshi la Nigeria vikisaidiw na ndege za vita baadaye vilizima uvamizi huo.
Mamlaka awali zilikana kuwa wasichana hao walikuwa wametekwa, zikisema kuwa walikuw wamejificha kutoka kwa wanamgambo hao.
Lakini baadaye wakakiri kuwa wasichana 110 walikuwa hawajulikani waliko baada ya uvamizi huo.





Msichana mwenye umri wa miaka 25, Anastazia Elias, mkazi wa Kata ya Kipindu wilayani Nkasi mkoani Rukwa, amenusurika kifo baada ya kuokolewa na polisi akituhumiwa kumuua mtoto wake baada ya kujifungua.
 
Wananchi wakiwa na silaha za jadi yakiwemo mawe walianza kumshambulia mwanamke huyo wakimtuhumu kumuua mwanawe wa kiume baada ya kujifungua ambapo alimviringisha na vipande vya khanga na kumuweka kwenye kikapu alichokificha chini ya uvungu wa kitanda chake.
 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea juzi saa nane mchana katika Kijiji cha Kipundu kilichopo mjini Namanyere.
 
Kamanda Kyando amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Polisi wilaya Nkasi na kwamba atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi wa tukio kukamilika. Wakizungumza baadhi ya wanawake  wamedai mtoto huyo alizikwa juzi usiku katika kaburi lililochimbwa ndani ya nyumba ambayo mama yake mzazi anaishi na bibi yake

Kwa mara ya kwanza Zari the Bossy Lady ambaye ni mama watoto wa msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Diamond Platinumz amefunguka kuhusu sababu za kuachana na C.E.O huyo wa kundi la Wasafi Classic Baby (WCB), amesema Diamond hakutegemea alichokipost kwani siku kabla ya kuachana walikuwa wamechuniana kwa takribani muda wa wiki tatu mfululizo, huku akiwa ameifungia simu yake, ”Block”.

Zari akiwa nchini Uingereza amepata nafasi ya kuzungumza na BBC  Swahili na kufunguka kila kitu kuhusu ishu nzima mpaka kufikia maamuzi hayo ya kutangaza kwenye akaunti yake ya instagram kuachana na Diamond katika siku ya wapendanao.

  ‘’Kwanza I didn’t think ali expect my post he didn’t see it coming ,nimekaa sana mda mrefu nikajifikiria vitu vingi nikasema unajua ni nini I need to post this, I  need to end this..tulikuwa tuna jaribu ku move forward kuhusu hiyo skendo eti amepata mtoto, lakini leo unasikia hivi unaona vile eti kukumbatiana na ma x kwenye public ni vitu vya kunidharirisha vitu vya kunifanya niwe very disrespected na watoto wangu’’, amesema Zari.

Zari amesema saivi hata akitembea kwa miguu kwenda kumuomba msamaha hawezi kumsamehe kwa sababu Imani juu yake imekwisha, na amesema kwa sasa hahitaji kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.

Ameongezea kuwa wale wanao dhani ni kiki hawajaachana Zari amesema ni kweli wameachana na tangu kusambaa picha za Diamoni akikumbatiana na  EX wake ambaye ni Madam  Wema Sepetu, Zari amesema alimzimia simu na hawakuweza kuongea kwa wiki tatu na kisha akaamua kuchukua uamuzi wa kuachana nae.

Zari pia amezungumzia mipango yake ya hivi sasa ambapo amesema atakuwa anafanya vitu vingi ikiwemo kuendesha biashara na kazi zake ambazo amekuwa akifanya ikiwemo kusimamia shule yake iliyopo Afrika Kusini, kufanya matangazo na hivi karibuni anakuja na kipindi chake sehemu ya pili ya show yake ijulikanayo kama reality show.



Vilio, simanzi na kupoteza fahamu kwa baadhi ya wanafunzi ni baadhi ya matukio ya huzuni yanayojitokeza katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), baada ya kuwasili mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa chuo hicho, Akwilina Akwiline.

Mwili wa mwanafunzi huyo unaagwa leo, Februari 22, 2018 katika viwanja vya chuo hicho.

Wanafunzi zaidi ya wanne aliokuwa akisoma nao Akwilina chuoni hapo ni kama hawaamini baada ya kushuhudia jeneza lenye mwili wake, huku wengine wakipoteza fahamu na kupewa huduma ya kwanza na Shirika la Msalaba Mwekundu.

Viongozi waliofika mpaka sasa katika viwanja vya NIT ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi; Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako; Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni; Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa na Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika.
 
Tayari ibada ya kuaga mwili wa mwanafunzi huyo imeanza.
 
 
 

MKRdezign

Blogger Widgets

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget