Zari
akiwa nchini Uingereza amepata nafasi ya kuzungumza na BBC Swahili na
kufunguka kila kitu kuhusu ishu nzima mpaka kufikia maamuzi hayo ya
kutangaza kwenye akaunti yake ya instagram kuachana na Diamond katika
siku ya wapendanao.
‘’Kwanza
I didn’t think ali expect my post he didn’t see it coming ,nimekaa sana
mda mrefu nikajifikiria vitu vingi nikasema unajua ni nini I need to
post this, I need to end this..tulikuwa tuna jaribu ku move forward
kuhusu hiyo skendo eti amepata mtoto, lakini leo unasikia hivi unaona
vile eti kukumbatiana na ma x kwenye public ni vitu vya kunidharirisha
vitu vya kunifanya niwe very disrespected na watoto wangu’’, amesema
Zari.
Zari
amesema saivi hata akitembea kwa miguu kwenda kumuomba msamaha hawezi
kumsamehe kwa sababu Imani juu yake imekwisha, na amesema kwa sasa
hahitaji kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.
Ameongezea
kuwa wale wanao dhani ni kiki hawajaachana Zari amesema ni kweli
wameachana na tangu kusambaa picha za Diamoni akikumbatiana na EX wake
ambaye ni Madam Wema Sepetu, Zari amesema alimzimia simu na hawakuweza
kuongea kwa wiki tatu na kisha akaamua kuchukua uamuzi wa kuachana nae.
Zari
pia amezungumzia mipango yake ya hivi sasa ambapo amesema atakuwa
anafanya vitu vingi ikiwemo kuendesha biashara na kazi zake ambazo
amekuwa akifanya ikiwemo kusimamia shule yake iliyopo Afrika Kusini,
kufanya matangazo na hivi karibuni anakuja na kipindi chake sehemu ya
pili ya show yake ijulikanayo kama reality show.
Post a Comment