Vilio,
simanzi na kupoteza fahamu kwa baadhi ya wanafunzi ni baadhi ya matukio
ya huzuni yanayojitokeza katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT),
baada ya kuwasili mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa chuo hicho, Akwilina
Akwiline.
Mwili wa mwanafunzi huyo unaagwa leo, Februari 22, 2018 katika viwanja vya chuo hicho.
Wanafunzi
zaidi ya wanne aliokuwa akisoma nao Akwilina chuoni hapo ni kama
hawaamini baada ya kushuhudia jeneza lenye mwili wake, huku wengine
wakipoteza fahamu na kupewa huduma ya kwanza na Shirika la Msalaba
Mwekundu.
Viongozi
waliofika mpaka sasa katika viwanja vya NIT ni Waziri wa Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi; Waziri wa Elimu, Profesa
Joyce Ndalichako; Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni;
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa na
Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika.
Tayari ibada ya kuaga mwili wa mwanafunzi huyo imeanza.
Post a Comment