TAMBI ZA HILIKI NA SUKARI


Chakula hiki ni kihisi kwa kupika, lakini ladha yake ni tamu. Mchanganyiko wa rangi unakupa hamu ya kula. Unaweza kula pamoja na nyama (kuku, sausage, mbuzi, ng’ombe) au salad ili kuongeza ladha na vilevile rangi tofauti za vyakula. Ni vizuri pia kama ukila chakula hiki kwa salad ya nyanya, pilipili hoho na karoti ambayo inaongeza appetite sababu ya mchanganyiko wa rangi mbalimbali.


MAHITAJI

  • Tambi 500g 
  • Sukari vijiko 2 vikubwa
  • Hiliki 3 au 5 Mafuta ya kupikia 1/4 lita

MAELEKEZO

Chakula hiki utapika katika sehemu mbili, ya kwanza ni kukaanga na ya pili ni kuchemsha. Kisha utachanganya ili kupata mchanganyiko maridhawa wa mlo kamili. Ni vizuri kama utafanya vyote wakati mmoja, ila kama huna nafasi jikoni unaweza kuanza na kimoja kisha ukamalizia na kingine.
  • Anza kwa kumenya hiliki, kisha hifadhi maganda.
  • Toa tambi kwenye packet, kisha gawa kwenye makundi mawili – kundi moja tambi za kukaanga na lingine za kuchemsha.
  • Anza kuandaa kama ilivyoelezwa hapa chini. Ni vizuri kama utafanya hizi hatua kwa pamoja ili tambi zipate kuiva kwa muda mmoja.
Tambi za Kukaanga
  • Bandika sufuria au kikaango cha mafuta jikoni, acha yachemke vizuri.
  • Mafuta yakishachemka, ongeza fungu moja la tambi ulizotenga (Za kukaanga). Acha kwenye mafuta kwa muda kiasi hazi zianze kubadilika rangi. Ni vizuri kama hutoacha tambi zibadilike sana rangi kuwa za brown, maana zitaungua na kutokuwa na ladha nzuri. 
  • Epue tambi mapema kupata rangi ya wastani. Zitakuwa zimeiva vizuri tu.
Tambi za kuchemsha
  • Bandika chungu au sufuria ya maji jikoni kwa ajili ya kuandaa tambi za kuchemsha.
  • Weka maganda ya hiliki kwenye maji ya moto ili kuweka harufu nzuri kwenye tambi. Baada ya dakika kama 5 unaweza kuchuja maganda ya hiliki na kubaki na maji yenye harufu ya hiliki.
  • Chukua kiasi cha tambi zilizosalia, weka kwenye maji ya moto, kisha ongeza sukari na hiliki.
  • Subiria tambi zichemke kutokana na muda ulioshauriwa - dakika 5 hadi 7 - ili zisiwe na kiini kigumu ndani. Hapo tambi zako zitakua zimeiva.
Changanya Tambi
  • Changanya tambi za kukaanga na tambi za kuchemsha pamoja. Katika hatua hii unapata mchanganyiko wa rangi tofauti za tambi, harufu nzuri ya hiliki na utamu wa sukari unamalizia.
  • Chakula chako kitakuwa tayari kwa kuliwa

Post a Comment

[blogger]

MKRdezign

Blogger Widgets

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget