KABEJI YENYE ROYCO


Mahitaji

  1. Kabeji nusu
  2. Kitunguu maji 1 kikubwa
  3. Royco kijiko 1 cha chai
  4. Mafuta ya kula vijiko 2
  5. Karoti 1
  6. Chumvi kijiko 1

Maelekezo

  • Andaa kabeji kwa kukata kwenye saizi unayopenda. Osha vizuri, chuja maji. Menya karoti, kisha changanya na kabeji.
  • Bandika sufuria jikoni, ikipata moto weka mafuta. Mafuta yakipata moto weka kitunguu maji huku unakoroga taratibu. Kitunguu kikiiva weka kabeji na chumvi. Pika kwa moto mkali kwa dakika 5. Weka royco na koroga kwa dakika 3 hadi 5 kisha epua.
  •  Jirambe na mboga tamu ya kabeji.
  •  Unaweza kula hii mboga na ugali, wali na vyakula vingine uvipendavyo.

Post a Comment

[blogger]

MKRdezign

Blogger Widgets

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget