Malkia Kipepeo

Latest Post



Mwanadada Irene Uwoya na mume wake Dogo Janja ambao kila siku hawaishiwi na drama katika  mitandao wanakuja tena kivingine na kuelezea jinsi mwezi mtukufu wa Ramadhani unavyodumisha mahusiano katika ndoa yao.

Irene anasema kuwa akiwa kama mke halali wa Abdul (janjaro) anahaki zote za kukaa na kutulia kipindi hiki cha ramadhan na kumpikia mume wake  kwa sababu hicho ni kitu alichozoea hata katika ndoa yake iliyopita.
 
"Kuhusu kufunga kwa upande wangu nilishazoea kwa sababu hata siku za nyuma za ramadhani nilikuwa nikifanya hivyo hivyo nilipokuwa na Ndiku na kwa sababu sasa hiv mimi ni mke halali kabisa wa Abdul basi nina haki ya kutulia na kumpikia mume wangu futari."-Uwoya




Mwanamuziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ameomba radhi baada ya ugomvi wake na Baba mtoto wake Mo J.

Gigy Money alimtolea maneno makali Ex wake ikiwemo kuweka wazi kwenye Interview aliyofanya na Millard Ayo kuwa mtoto wake Myra sio wa Mo J kwani alikuwa na mwanaume mwingine.

Gigy Money na Ex wake Mo J walirushiana maneno makali baada ya Gigy kumtuhumu kuwa hakuwa akimtunza kipindi cha ujauzito na kudai alihama na kila kitu baada ya kuachana.

Baada ya sakata hilo Mo J aliongea na vyombo vya habari na kudai kuwa ana uhakika kuwa mtoto wao ni wa kwake ingawa Gigy kwa ajili ya hasira anampa  mtoto mpenzi wake wa sasa.

Baada ya povu hilo Gigy Money ameibuka na kuomba radhi kwa maneno aliyoongea huku akidai ilikuwa ni hasira

Mama mzazi wa aliyekuwa msanii wa Bongo movie Marehemu Steven Kanumba, Mama Kanumba ameibuka na jipya tena huku safari hii akisema anatamani kwenda jela kumuona Lulu.

Mama Kanumba hakuwa na uhusiano mzuri na Lulu kwani mpaka a nafungiwa walikuwa kama wana ugomvi fulani huku Mama Kanumba alidai sababu kubwa ni Lulu kumtupa mama huyo na kutomjali kwa lolote.

Miezi michache iliyopita Muigizaji wa Bongo movie Lulu Michael alifungwa gerezani kwa miaka miwili baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake Steven Kanumba.

Baada ya Lulu kufungwa Mama Kanumba hakusita kuonyesha furaha yake juu ya Lulu kufungwa na baadae alipoulizwa endapo ana mpango wa kwenda kumtembelea Lulu gerezani alisema hajui mpaka afanye mazungumzo na Mungu wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Mwananchi Communications, Mama Kanumba ameibuka na kusema anatamani kwenda kumuona Lulu jela:

"Tangu Lulu kahukumiwa nimekuwa nikipokea lawama na watu kunitusi kuwa mimi ndio sababu, na kusahau ya  kwamba mimi nilishamsamehe kama binadamu na siye niliokuwa mlamlamikaji katika kesi hiyo isipokuwa alishitakiwa na serikali”.

Lakini Mama Kanumba amesisitiza kuwa yote yaliyotokea anamuachia Mwenyezi Mungu kwani yeye kufungwa hakuwezi kumrudishia mtoto wake ambaye amekwisha tangulia mbele ya hali.


Mahitaji

  • Nyama  - kilo 1
  • Mafuta ya kula - 1/2 lita
  • Chumvi 
  • Ndimu / limao 1
  • Tangawizi  - 1
  • Kitunguu saumu  - 1
  • Viazi - 6
  • Viungo vingine upendavyo kwenyewaweza kuweka

Maelekezo

  • Tayarisha nyama yako - kata, osha.
  • Weka limao, ndimu au vinegar kwenye nyama, ichanganye ili limao lichanganyike vizuri.
  • Ponda tangawizi kwenye kinu, iwe laini.
  • Ponda kitunguu swaumu kwenye kinu, ilainike vizuri.
  • Weka viungo - chumvi, tangawizi na kitunguu saumu kwenye nyama. Changanya nyama ili viungo vipate kuchanganyika vizuri. Acha nyama ikae kwa dakika 45 kwenye jokofu ili viungo viingie vizuri. Jinsi viungo vinavyokaa vizuri kwenye nyama ndio inazidi kunoga.
  • Bandika sufuria au kikaangio jikoni, weka mafuta kiasi. Subiria yapate moto.
  • Weka nyama kwenye mafuta.  Koroga ili ichanganyike vizuri na mafuta kisha funika sufuria au chungu na mfuniko. 
  • Geuza geuza nyama kila mara ili kuzuia isigande kwenye chombo cha kupikia. Subiria hadi iive.
  • Angalia kama nyama imeiva. Unaweza kuongeza pilipili manga ya unga ili kuleta ladha tofauti kwenye nyama.
  •  Unaweza kutenga na kula.
  •  Ni vizuri ukala kwa kachumbari nzuri pamoja na kinywaji upendacho au chakula chochote ukipendacho

 
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu amesema ana kila sababu ya kuzungumza japo kwa kifupi jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na serikali katika kuimarisha usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini.

Makamu wa Rais amesema kuwa serikali ina sera kuendeleza wanawake,huku akisema kuwa sheria ya ardhi za mwaka 1999 ambazo husimamia haki za wanawake katika kumiliki ardhi.

"Leo katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Mimi kama mwanamke na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nina kila sababu ya kuzungumza japo kwa kifupi jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na serikali katika kuimarisha usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini.

"Serikali inayo Sera ya kuendeleza Wanawake, Sheria za ardhi za mwaka 1999 ambazo husimamia haki za wanawake katika kumiliki ardhi.

"Sera ya elimu bure inayotekelezwa na serikali ya Awamu ya Tano imetoa fursa kwa watoto wengi wa kike kuandikishwa shuleni.

"Kuboreshwa kwa huduma za kijamii kama vile kujengwa zahanati na vituo vya afya na usambazaji wa maji vimempunguzia mwanamke usumbufu na hivyo kumpa muda wa kutosha kufanya shughuli za maendeleo.

"Usambazaji umeme vijijini kwa kiasi kikubwa umesaidia wanawake wengi kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato.

"Uwezeshaji wa Wanawake kwa kuwapatia asilimia 5 ya mapato ya halmashauri na asilimia 30 ya zabuni za halmashauri kumewawezesha wanawake wengi kufanya biashara na hatimaye kuwa na uhakika wa kipato .

"Serikali kuendelea kuhimiza taasisi za kifedha kutoa mikopo yenye riba nafuu ili kuwawezesha wanawake wengi kunufaika na mikopo hiyo.

"Kurasimisha vikoba pamoja na kuwashawishi wanawake wengi zaidi kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuweza kunufaika na mafao na mikopo itolewayo na taasisi hizo.

"Kauli Mbiu:Kuelekea Uchumi wa Viwanda tuimarishe usawa wa kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini."



JESHI la Polisi mkoani Mwanza, linamshikilia Soli Mkanzabe (24), mkazi wa mtaa wa Nyegezi kwa tuhuma za kumnajisi mtoto wa miaka minne (jina limehifadhiwa) na kumsababishia majeraha na maumivu makali katika sehemu za siri.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna (DCP) Ahmed Msangi, katika taarifa aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari, alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo juzi majira ya saa 10 jioni katika maeneo ya mtaa wa Password kata ya Nyegezi, Nyamagana mkoani hapa.

“Inasemekana mtuhumiwa alikuwa akiishi jirani na nyumbani kwao mtoto. Inadaiwa kuwa majira tajwa hapo juu, mtuhumiwa alifika nyumbani kwao mtoto na kumkuta akicheza na wenzake kisha alimwita waende wote chumbani kwake.

Mtoto alimfuata mtuhumiwa na kwenda naye chumbani na baadaye mtuhumiwa alifanyia mtoto ukatili wa kumbaka na kumsababishia maumivu makali katika sehemu za siri huku mtuhumiwa akimwonya mtoto kuwa asiseme kwa mtu yeyote juu ya jambo hilo,” alisema DCP Msangi katika taarifa hiyo.

Msangi alisema baada ya mtoto kufanyiwa ukatili huo, alikaa kimya bila kumwambia mtu yeyote hadi mama yake aliporejea kutoka kazini.

Kamanda Msangi alisema wakati mama yake akienda kumwogesha, ndipo alipogundua kuwa mtoto amefanyiwa unyama huo kisha alitoa taarifa kituo cha polisi.

Alisema baada ya kutoa taarifa, polisi walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa.

Kutokana na kumkamata huko, DCP Msangi alisema polisi wako katika upelelezi na mahojiano namtuhumiwa na kwamba uchunguzi ukikamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Kuhusu mtoto huyo, Msangi alisema alipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana na kwamba hali yake inaendelea vizuri.

MKRdezign

Blogger Widgets

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget